Header Ads

Kongamano la Msafara lawajenga Vijana Wengi

 Msanii wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielezea jinsi Sanaa inavyoweza kumkomboa kijana,na kutoa mifano ya baadhi ya wasanii walioanzia chini na sasa wanamafanikio makubwa.
Baadhi ya vijana wakionesha ishara ya ushindi.
Alphonse Matata ambaye anajihusisha na kilimo pia Mjasiliamali kupitia ufugaji wa nyuki akielezea safari yake ya mafanikio ,na kuwashauri vijana wasingoje kuajiliwa bali wawe wabunifu na kujiunga katika ujasiliamali, jana tarehe 4.12.2015.

 MC Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji.
 
Mjasiliamali Maarufu na Mtoa ushauri wa biashara na mambo mbalimbali James Mwang'amba, alitoa Historia ya Maisha yake na kutoa siri tatu za mafanikio ambazo ni kuwa na maono ya maisha bora ya baadae, kujifunza kwa kupitia njia mpya ya Teknolojia mfano youtube na kuwa na mtu ambaye unahisi unaweza ukajifunza kwake. 
 Baadhi ya vijana wakifuatilia Kongamano hilo.
 Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake 2002-2003 na kuchezea mpira timu hiyo kwa Miaka 15 mpaka anastaafu mwaka huu Esther Chabruma akielezea namna mchezo wa Mpira wa Miguu ilivyoweza msaidia mpaka hapa alipofikia na kuwasihi vijana wasikate tamaa maana kila jambo lina wakati wake.
 Baadhi ya vijana wakiwa wanasikiliza kwa makini vijana wenzao wakielezea safari zao za mafanikio.
 Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitaponda Ahadi, akielezea kuhusu elimu na changamoto alizo zipata wakati wa akiwa Shule mpaka ndoto yake ilivyotimia ya kuja kusoma chuo kikuu na kuwa kiongozi, amewasihi vijana wenzake wasikate tamaa wafanye bidii katika masomo watafikia malengo.
  Major Mbuya mtaalam wa kuendesha Baiskeri na mwanzilishi wa waendesha Baiskeri Tanzania, akielezea jinsi ubunifu ulivyo msaidia mpaka sasa amefanikiwa.
 Hassan ally kijana mjasiliamali akieleza namna alivyoweza kubadilisha taka na kuwa Bidhaa ambayo inaweza kutumika tena kwa matumizi mengine pia, ameelezea mpango wake wa kuanza kujenga nyumba kwa kutumia bei nafuu.

Vijana mbalimbali wamejitokeza katika kongamano la msafara kusikiliza baadhi ya vijana wenzao ambao wametoa historia zao kuhusu walipotokea mpaka wamefanikiwa kufika hapo walipofikia na kuwatia moyo vijana wengine wasikate tamaa kwa sababu mafanikio yapo.

Msafara ambao unalenga kuibua na kurudisha ndoto za vijana katika sekta zote kwa kutambua kuwa kila eneo lina mchango mkubwa katika mafanikio na maendeleo ya vijana. Wazungumzaji tofauti tofauti walijikita katika maeneo makuu yafuatayo Sayansi na Teknolojia,Kilimo, Biashara, Sanaa na usanii, Elimu, Uongozi, Michezo, utunzaji Mazingira, haki sawa za kijinsia pamoja na harakati.

Maeneo hayo yalikuwa ni nguzo kuu ya kufanya vijana kuwa na fursa ya kukabiliana na changamoto za kimaisha katika kufikia mafanikio na malengo yao. Katika safari hii ya Msafara matukio mbalimbali yatafanyika ikiwemo kuwaleta vijana wa rika moja wenye umri wa miaka 15-24 ili kuwaleta kwa pamoja wapate kujifunza kutoka kwa wengine waliofanikiwa, wenye fani mbalimbali/Taaruma zao, hii itawajengea ujasili wengine katika kufikia mafanikio yao.

Progamu hii inaendeshwa na muungano wa Mashirika na Makundi Matano yaliyopo hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na DARUSO, YouthCAN, NGAO YOUTH na Young Feminist Forum na inaratibiwa na Oxfam Tanzania, msafara itakuwa ni moja ya fursa kwa vijana kutangaza na kuonesha ubunifu wao na mafanikio waliyofikia kimaisha ingawa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali. 

Safari ya msafara itaendelea Ifakara mkoani Morogoro tarehe 12.12.2015

No comments

Powered by Blogger.