Bonanza la MADESHO DAY lafanyika
Timu ya Ushrika wakijandaa kuvuta kamba katika bonanza la kumbukumbu ya Mwenyekiti wa kwanza wa klabu ya Moshi veterani Marehemu Madesho Moye. |
Timu za Maveterani wa KIA na Kitambi noma ya Arusha wakioneshana kazi katika kuvuta kamba. |
Mashindano ya Mbio za mita 100 pia zilikuwa kivutio hapa ,Salvatory Mtanange akionesha uwezo wa kukimbia mita 100 ambapo alifanikiwa kushinda. |
Mwamuzi maarufu wa mchezo wa kukimbiza kuku nchini akiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huo. |
Kikosi cha timu ya Ushirika Veterani. |
Kikosi cha wachezaji wa timu ya Kitambi noma. |
Amosi Makala akijaribu kutaka kupita walinzi wa timu ya Ushirika Veterani. |
Amosi Makala akijiandaa kupiga mpira wa adhabu . |
Baadhi ya Mashabiki wa timu mbalimbali za maveterani zilizoshiriki Bonanza la kumbukumbu ya Mwanzilishi wa klabu ya Moshi Veterani,Marehemu Madesho Moye. |
Mshambiliaji wa klabu ya Ushirika Veterani Tumaini Masue akijaribu kutafuta njia za kutaka kumpita mlinzi wa timu ya Kitambi noma. |
Masue akijaribu kuzuia mara baada ya kushindwa kupita . |
Mke wa Marehemu Madesho,Shufaa Madesho alikuwepo uwanjani hapo kufuatilia Bonanza hilo. |
Mke wa Marehemu Madesho ,Shufaa Madesho akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika Bonanza hilo wakifuatilia mchezo. |
Zawadi zikatolewa kwa mchezaji Cunbert Ngambira wa timu ya Maveterani wa KIA baada ya kushinda mbio za Mita 100 kwa wenye umri wa miaka 30-40. |
Zawadi zikatolewa kwa mshindi wa mbio za Mita 100 Salatory Mtanange wa Moshi veterani kwa wakimbiaji wenye umri kati ya miaka 40 na 50. |
Mshindi wa pili kwa upande wa mpira wa Miguu timu ya Ushirika Veterani ,wakakabidhiwa kikombe,nahodha wa timu hiyo Erick akapokea kwa niaba ya timu. |
Washindi wa pili timu ya Maveterani ya Best Maridadi ,wakakabidhiwa kikombe ,kikapokelewa na Ismail . |
Washindi wa kwanza kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Maveteran wa njia panda ya Ulaya KIA,wakakabidhiwa kikombe na mgeni rasmi ,Amosi Makala. |
KIA wakifurahia kikombe chao cha kwanza tangu kuanzishwa kwa timu hiyo. |
Mgeni rasmi katika Bonanza hilo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi. |
Mke wa Marehemu Madesho akizungumza katika Bonanza hilo. |
Baadhi ya ndugu waliofika katika Bonanza hilo. |
Post a Comment