Header Ads

Mkuu wa Wilaya ya KILOLO Bi Asia Abdallah aonya Wanaozembea Zoezi la Usafi

Mkuu   wa  wilaya  ya  Kilolo Asia Abdulah ametangaza  kuwachukulia  hatua  kali  wananchi  watakaopuuza agizo la   Rais Dr  John Magufuli na   kufanya usafi  wa mazingira  yanayowazunguka  kila juma  la mwisho la mwezi .

Huku  akipiga  marufuku   kilimo  cha mahindi nje  ya ofisi  yake  kuwa kuendelea  kulima mahindi na mazao yanayozidi  futi tatu  katika eneo   linalozunguka  ofisi  yake ni moja ya  uchafuzi  wa mazingira na  kuwa kuanzia   sasa mazao marefu katika  maeneo yote  yanayozunguka ofisi za  umma  ni marufuku .

Mkuu  huyo  wa  wilaya alitoa kauli  hiyo  juzi  baada ya  kuongoza oparesheni  ya usafi kwa watumishi  wa Halmashauri ya  Kilolo na wanafunzi  wa   shule ya sekondari  Kilolo  kufanya usafi maeneo ya jengo la  ofisi  ya  mkuu  wa   wilaya ya  kilolo  jengo  ambalo nyoka walikuwa wakitishia usalama  wa  watumishi  wa  ofisi  hiyo  kutokana na jengo   hilo  kuzungukwa na  nyasi  ndefu na  vichaka kwa  zaidi ya miaka 10 .



Akizungumza  baada ya  zoezi  hilo  mkuu  huyo  wa  wilaya  aliwapongeza  wakuu  wa idara  katika halmashauri ya  Kilolo pamoja na  wananchi  ambao  waliitikia  wito  wa  kufanya  usafi    huku  akisema  idadi ya  wananchi  waliofika  kufanya  usafi  hajafurahishwa nao  kwani  ni  wananchi  wachache  ambao   walitoka  kufanya  usafi  pamoja na  gari ya matangazo   kupita  mitaani kabla  ya  siku ya  usafi  na  kuhamasisha  wananchi  kushiriki zoezi hilo .
Mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo Bi Asia  Abdalah  akishirikiana na  wanafunzi  wa  shule  ya  Sekondari Kilolo  kufanya  usafi  wa  kufyeka  nyasi nje  ya  ofisi ya  mkuu  huyo wa  wilaya  juzi kama  sehemu ya  kuitikia agizo la  Rais Dr John Magufuli la  kila jumamosi ya  mwisho  wa mwezi  ni  siku ya  usafi.
Jengo  la ofisi  la ofisi ya  DC Kilolo.
Kaimu  mkurugenzi  wa  Halmashauri ya  Kilolo  akishiriki  usafi nje ya  ofisi ya  DC  Kilolo.
Watumishi  Kilolo  na  wanafunzi   wakifanya  usafi  ofisi ya  mkuu wa wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa.

Mtumishi  wa Halmashauri ya  Kilolo  akichoma moto nyasi  zilizokusanywa.

No comments

Powered by Blogger.