Header Ads

MSAADA: Mkazi wa Dodoma ROBERT LAURENT Atoweka Katika Mazingira ya Kutatanisha

Mkazi wa kijiji cha Kabare kata ya Uwarama wilaya ya Kakonke, Robert Laurent (35) ametoweka nyumbani kwake Dodoma Makulu katika mazingira ya kutatanisha.

kwa mujibu wa Shemeji yake, Mchungaji Philip Kayanda, amesema kuwa Laurent alikuwa ametokea Zanzibar na kuelekea Kahama lakini alipofika hapa Dodoma aliteremka na kuelekea nyumbani kwao eneo la Dodoma makulu ambako alitoweka kusikojulikana.

 Mchungaji Kayanda alisema kuwa shemeji yake huyo ana matatizo ya  akili.

Laurent ambaye rangi yake  maji ya kunde amesema kabla  ya kujachanganyikiwa akili ,alikuwa anafanya kazi ya uchungaji katika kanisa la FPCT huko kijijini kwao Kabare mkoa wa Kigoma  ikiwemo na  Zanzibar.

Amesema jitihada za kumtafuta kwa ndugu, jamaa na marafiki zimefanyika bila mafanikio na tayari wametoa taarifa kituo cha polisi kati cha Dodoma na kufungua jalada namba RB/DOM/8409/2016.

Ameomba kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu ama apige simu  namba 0688 - 688229,0788 – 669300  au 0655 – 090820.

No comments

Powered by Blogger.