Header Ads

Rais Dkt JOHN MAGUFULI ashiriki Mazishi ya Mzee SELEMANI MRISHO KIKWETE Kijijini Msoga

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mama Salma Kikwete wakiwa msibani kwa kaka yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mama Asha Bilali, Mama Khadija Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mama Asha Seif Ali Iddi. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea hela ya utani toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi hela ya utani kwa mkaazi wa Chalinze ambaye ni Msukuma Bwana Luhende baada ya kuipokea toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na 
Wasukuma ni watani.
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinayang Bw. Khamis Mgeja akiongea na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais MStaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete,  kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016

PICHA NA IKULU


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshiriki maziko ya Marehemu Selemani Mrisho Kikwete ambaye ni Kaka wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete yaliyofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo katika kijiji cha Msoga, Wilaya ya BAgamoyo Mkoani Pwani.

Mzee Selemani Mrisho Kikwete alifariki dunia tarehe 01 Machi, 2016 huko nchini India ambako alipelekwa kwa ajili ya kupata matibabu ya saratani.

Pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Marais wastaafu Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi na Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samwel Malecela, Viongozi wa dini na siasa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Akizungumza kabla ya maziko, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na familia yake tangu wakati wa kuuguza, na hatimaye maziko ya kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete.

"Tumefarijika sana kwa kuwa nasi wakati wote wa kuuguza na leo siku ya maziko, nakumbuka pale wewe mwenyewe ulipohakikisha unasimamia matibabu ya kaka yangu alipokuwa nchini India" Amesema Rais Mstaafu Kikwete.

Aidha, Rais Kikwete amewashukuru viongozi wote na wananchi waliojitokeza katika mazishi ya Marehemu Kaka yake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
05 Machi, 2016


No comments

Powered by Blogger.