Header Ads

Mke wa Rais Mama JANETH MAGUFULI awataka Wadau Kujitokeza kusaidia Wazee na watu Wasiojiweza

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini Mwanza kushiriki zoezi la utoaji wa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiangalia burudani ya ngoma alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akimkaribisha Mama Janeth Magufuli kuongea na Wazee na pia kuwahakikishia wazee kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia katika ahadi zake hasa katika kuhakikisha wazee wanapata huduma bila usumbufu.
22 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika Kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza  cha Bukumbi Mkoani Mwanza wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali na kuyashukuru mashirika, Taasisi za serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutoa misaada hiyo ikiwemo Mchele, Unga, Maharage, Mafuta ya kupikia, mashine za kufulia pamoja na solar panel pia akatoa rai kwa wadau wengine kujitolea kusaidia wazee na watu wasiojiweza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee katika kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.

No comments

Powered by Blogger.