Header Ads

Ujumbe wa Benki ya Dunia Watembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria Viwanja vya Mnazi Mmoja DAR ES SALAAM

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird aliyetembelea  Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es salaam leo, Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Kisekta wa Benki ya Dunia Bw. Waleed Maliki.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (kushoto) alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Malalamiko na Maadili la Mahakama katika viwanja vya Mnazi Mmmoja leo.
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kushoto) akionesha ugeni kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania michoro ya majengo mapya ya Mahakama yanayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini . Kutoka kulia  ni  Bw. Larbi George Addo kutoka Benki ya Dunia akifuatiwa na  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kutoka kulia) na  Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Kisekta wa Benki hiyo Bw. Waleed Maliki.
Afisa Magereza kutoka Jeshi la Magereza jijini Dar es salaam, Rose Odemba (kulia) akitoa Ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (kulia) kuhusu Utaratibu wa kuwaachia wafungwa kwa masharti baada ya kutumikia 1/3 ya vifungo vyao magerezani (PAROLE) walipotembelea banda la Maonesho la Jeshi la Magereza katika viwanja vya Mnazi mmoja leo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama ya Tanzania Bi. Wanyanda Philip Kutta akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (kulia) alipotembelea Maonesho ya Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya Wananchi waliotembelea mabanda ya maonesho ya Wiki ya Sheria nchini katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakiendelea kupatiwa msaada wa kisheria katika masuala mbalimbali.

No comments

Powered by Blogger.