Header Ads

Ziara ya Naibu Waziri SELEMANI JAFO Katavi yamuingiza Matatani Afisa Mipango Miji

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi),Selemani Jafo ameendelea na ziara yake leo mkoani katavi ambapo amemuagiza Afisa Tawala wa Mkoa wa Katavi kuunda timu ya uchunguzi ili  kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa Afisa Mipango miji wa Manispaa ya Mpanda ambapo anatuhumiwa kuchukua maeneo ya wananchi bila utaratibu.

Jafo katika ziara hiyo ametembelea wilaya ya Tanganyika na wilaya ya Mpanda.

Katika wilaya ya Tanganyika aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda vijijini Moshi Kakoso ambapo alikagua kukagua mradi wa Maktaba ya shule ya sekondari Kabungapamoja na mradi wa Maji katika jimbo la mpanda vijiji.

Naibu Waziri Selemani Jafo akikagua ujenzi wa stendi ya mabasi Manispaa ya Mpanda.
Kwa upande wa Manispaa ya Mpanda alifanikiwa kukagua hospitali ya wilaya ya Mpanda pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa.

Hata hivyo Jafo ilihitimishwa kwa kufanya mkutano na watumishi wote wa Halmashauri ya Mpanda pamoja na Manispaa ya Mpanda katika  ukumbi wa idara ya maji uliopo mjini Mpanda.

Naibu Waziri ameendelea kutoa maelekezo ya utendaji kazi kwa watumishi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia dhana kubwa ya mabadiliko.

Katika majumuisho hayo, Jafo hakufurahishwa na tabia ya baadhi ya watumishi wenye tabia ya ubadhirifu wa fedha za umma na kutowajali wananchi.
Naibu Waziri Jafo akiwa na walimu wa shule ya sekondari Kabunga.
Kuhusu Afisa mipango huyo, Jafo amesema amewapa fedha kidogo wananchi wenye ardhi nje ya utaratibu kisha kuyauza maeneo hayo kwa gharama kubwa kwa matajiri.

Kadhalika, Jafo amesema Afisa huyo analalamikiwa kuhodhi viwanja kadhaa ndani ya Manispaa hiyo kwa kutumia nyadhifa aliyonayo.

“Kutokana na tuhuma hizo namuagiza Katibu tawala mkoa(RAS) Katavi kuunda timu ya uchunguzi kisha kuwasilisha ripoti Ofisi ya Rais Tamisemi kwa hatua za kinidhamu endapo itabainika ukweli wa tuhuma hizi,”alisema Jafo.
Eneo la stendi ya kisasa ya mabasi ya Manispaa ya Mpanda Linavyoonekana kwa sasa.
Naibu Waziri Selemani Jafo akikagua ujenzi wa stendi ya mabasi Manispaa ya Mpanda.
Naibu Waziri Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Kabunga.
Ukaguzi wa Stendi ya mabasi Ukiendelea......

No comments

Powered by Blogger.