Header Ads

Wanamichezo waaswa Kutotumia Dawa za Kuongea nguvu Katika Michezo


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw. Maharage Chande  akishukuru Serikali kwa fursa ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo wakati wa hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na wanamichezo na wadau wa michezo  katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaoenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo  katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Baadhi ya wadau wa michezo wakifuatilia yanayojiri katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  kwenye mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi bendera kwa timu ya Tanzania inayoenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil  leo Agosti 1, 2016.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura( katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Tanzania inayoenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 nchini Brazil  leo Agosti 1, 2016 wa pili kulia waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo prof Elisante Ole Gabriel.


Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura( katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo waliowahi kushiriki mashindano ya Olimpiki  leo Agosti 1, 2016 kulia waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa michezo na wadhamini wa timu ya Olimpiki ya Tanzania  mara baada ya kuiaga timu hiyo inayoenda kushiriki mashindano ya Olimpiki nchini Brazil leo Agosti 1, 2016.


Wanamichezo nchini wameaswa kutojihusisha na matumizi ya dawa au mbinu za kuongeza nguvu katika michezo ili kuepuka na madhara yanayojitokeza ikiwemo kuzorotesha sekta ya michezo.


Wito huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akiwaaga wanamichezo wanaoenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.


Mhe. Anastazia Wambura amesema kuwa wanamichezo wengi duniani kwasasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu mwilini katika michezo mbalimbali.


“Niwatake wachezaji,madaktari na viongozi wa michezo mbalimbali kuhakikisha kuwa hakuna mchezaji anajejihusisha na vitendo vya aibu na kwa pamoja tuungane na kupinga jambo hili kwa kujali afya na ushindani uliopoa” alisema Mhe. Anastazia.


Aidha amewataka viongozi wote wa michezo, waalimu na madaktari wa michezo kuungana kwa pamoja kupiga vita matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni kwa kutoa elimu kwa wanamichezo wao na wasisite kutoa adhabu kali pale inapothibitika mwanamichezo amejihusisha na matumizi ya dawa hizo.


Kwa upande wake katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi ameahidi kutekeleza suala hilo kwa kutoa elimu kwa waalimu na wanamchezo juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za mwili katika michezo.

No comments

Powered by Blogger.