Header Ads

Mnada wa TANZANITE kufanyika Jijini Arusha wiki Hii

Na Zuena Msuya, Arusha

Wizara ya Nishati na Madini inafanya mnada wa madini ya Tanzanite kwa mara ya kwanza yaliochimbwa kutoka migodi ya kampuni tano za wafanyabiasha wa madini hayo katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiko Mkoani Manyara.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo  wakati wa mchakato wa kupata wafanyabiashara watakaoshinda zabuni ya kununua madini hayo kutoka Mataifa mbalimbali Duniani wakiwemo watanzania.

Kalugendo alisema utaratibu  wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei halisi inayoendana na soko la dunia.

Mhandisi Juma Lunda( kulia) akimuelekeza mmoja wa wanunuzi wa madini ya Tanzanite kujaza fomu za kushiriki zabuni ya kununua madini hayo.

Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao.

Akizungumzia mnada huo, Kalugendo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO) pamoja Wizara ya Nishati na Madini, kwa lengo la kusimamia haki ya kila mhusika wa madini hayo.

"  Madini ya Tanzanite yanathamani ya fedha nyingi sana,kwa usalama wa wanunuzi na wauzaji, Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hilo ili kujihadhari na watu wasio waaminifu," alisema Kalugendo. 
Vifaa vinavyotumika kuhifadhi Madini ya Tanzanite.

Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utaratibu huo ili uweze kuleta tija zaidi kwa Watanzania.

Utaratibu huo ni wa kaiwaida kwa nchi zenye madini ya namna hii kama vile Zambia( emerald),Zimbabwe( Almasi) pamoja na Afrika kusini( almasi).

Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Agosti 12 mwaka mkoani Arusha. 
Sehemu inayotumiwa na wauzaji pamoja na wanunuzi kujiridhisha kwa kupima thamani ya madini ya Tanzanite kabla ya kufikia muafaka wa bei. 
Mkurugenzi wa Uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo( wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite wakati wa zoezi la kumpata mshindi wa zabuni ya kununua madini ya Tanzanite. 
Mnunuzi wa madini ya Tanzanite Macmillan Njau( kulia) akijiridhisha kwa kupima thamani ya madini hayo kabla ya kununua, Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Franone Mining & Gem Company, Onesmo Mbise(katikati) ambaye ni muuzaji wa madini ya Tanzanite na Elia Benyamin( kushoto) Mnunuzi wa Madini.
Mthaminishaji Madini ya Almasi wa Serikali Edward Rweyemamu (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau wa Madini ya Tanzanite( kushoto), Sekretari wa kituo cha Jimolojia ( TGC)Halima Hussein( wapili kulia) na Zainab Napacho(kulia)kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania( TMAA).

No comments

Powered by Blogger.