Header Ads

Milioni 292 zatolewa kwa Kaya Masikini Wilaya ya ILALA

Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mwaluma Msofe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wakunusuru kaya masikini muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa fedha hizo kuanza katika mitaa 74 ya Manispaa hiyo leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kimanga - Darajani, Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala wakisubiri zoezi la ugawaji wa fedha kwa kaya masikini kuanza leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wakunusuru kaya masikini, Ayubu Kabeta akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha za kujikimu leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga - Darajani, Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala, Chacha Mwenge akiendelea na zoezi la kuhakiki majina ya wanufaika wa mpango wa TASAF katika mtaa wake leo tarehe 09/08/2016 Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.