Header Ads

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU Kuongoza Sherehe za NANE NANE Kitaifa, LINDI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mstahiki Meya wa Lindi mjini Ndugu Mohamed Liumbwe mara baada ya kuwasili mkoani Lindi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha   Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa  niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli.


Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI Godfrey Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.


Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Hamad Rashid.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu wakati wa mapokezi na Vijana wa mkoa wa Lindi .

 Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.

 Wakina Mama wa mkoa wa Lindi wakimuimbia nyimbo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mapokezi mkoani hapo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ndogo mkoani Lindi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu mara baada ya kuwasili kwene Ikulu ndogo mkoani Lindi wengine pichani ni Waziri wa Kilimo Maliasili na Uvuvi  wa Zanzibar Mhe.Hamad Rashidi  (kulia) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa.
                                            


No comments

Powered by Blogger.