DAWASCO yazidi Kumchefua Naibu Waziri wa Mazingira LUHAGA MPINA
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Bw. Boniventure Baya kumuandikia hati ya zuio ya muda wa siku saba
mkurugenzi wa kampuni ya Maji safi na Maji taka jijini DarEs Salaam na Pwani
DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja
ya Kueleza kwa nini kampuni hiyo
imetelekeza miundombinu yake ya majitaka na kupelekea uchafuzi wa mazingira
katika jiji la Dar Es Salaam.
Akitoa Agizo Hilo
Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa mwiki wakati wa majumuisho wa ziara yake ya
ukaguzi wa viwanda, mazingira na miundombonu ya DAWASCO na DAWASA, NAibu Waziri
Mpina alisema hati hiyo itamtaka Mkurugenzi huyo wa DAWASCO kueleza kwa nini
kampuni hiyo haitibu maji yatokayo
viwandani huku ikiendelea kupokea fedha toka viwandani na kuachia maji kusambaa
katika makazi ya watu.
Mpina Alisema kuwa DAWASCO wamekuwa wakipita katika viwanda
mbali mbali nchi na kutoza fedha za uzalishaji maji taka bila kuyapima maji
hayo na kuelekeza katika miundo mbinu mibovu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akimsikiliza Afisa wa kiwanda cha azam juisi mara baada kufanya ziara katika kiwanda hicho. |
Katika ziara hiyo ya siku nne, Naibu Waziri waziri aligundua
kuwa miundombinu mingi ya DAWASCO iko katika hali mbaya, huku walinzi wa miundo
mbinu hiyo wakifanya kazi katika mazingira hatarishi kwa afya zao kwa kukosa
vifaa vya kujikinga akitolea mfano kituo cha ku pump maji taka cha gymkhana
kinachopeleka maji taka katika bomba kubwa la majitaka baharini.
“Hati hiyo atakayoandikiwa mkurugenzi wa DAWASCO itamtaka
atueleze kwa nini hali ya miundombinu ipo hivi, kwa nini hawayatibu maji
yanayotiririka kwa wananchi huku wanapokea fedha toka katika viwanda, na kwa
nini wanatiririsha maji taka katika mto msimbazi bila kuyapima.” Alisema.
Akitolea Mfano kiwanda cha SAdoline kinachotengeneza Rangi,
alisema kiwanda hicho kimekuwa kikiwalipa DAWASCO zaidi ya shilingi milioni
moja kwa mwezi kwa ajili ya huduma ya uondoshwaji wa maji taka kupitia
miundombinu ya DAWASCO.
Aidha alisema katika kiwanda cha kutengeneza vinjwaji laini
cha AZAM kilichopo vingunguti, DAWASCO imekuwa ikipokea zaidi ya shilingi
milioni tatu kwa mwezi kwa ajili ya huduma hiyo lakini DAWASCO wamekuwa
wakipitisha maji hayo katikati ya makazi ya watu na kwenda kuyatitirisha katika
mto msimbazi jambo ambalo kisheria ni kosa.
“Hakuna huduma yoyote ya kutibu maji inayofanywa na DAWASCO
huku wamekuwa wakiendela kupokea pesa katika viwanda, miundombinu yao ni
mibivu, mabwawa ya kuhifadhia maji taka yamekuwa yakitirirsha maji hayo katika
makazi ya watu, kiukweli nahitaji maelezo ya kutosha kutoka DAWASCO.” Alisema
Mpina.
Kwa upande wake Mratibu wa mazingira wa kanda kutoka NEMC Bw.
Jaffari Chimgege alisema kuwa kutokana na ubovu wa miundombinu ya DAWASCO hali
ya jiji la Dar Es Salaam imekuwa chafu.
Alisema kunahitajika kazi ya ziada kurekebisha miundombinu
hiyo kwani hali hii ikiendelea wananchi watakuwa hatarini kupata magonjwa hivyo
ni lazima kazi ya ziada ifanyike.
“Inatupasa kila mtu kjutimiza wajibu wake kwa watu wa
viwanda,wananchi na DAWASCO kuhakikisha maji yanayotiririka yanakuwa yamepimwa
na kuonyesha kama hayana madhara yoyote kwa binadamu na sio kuacha maji taka
kutirirka katika makazi ya watu, hii ni hatari tunahatarisha afya za
watanznaia.” Alisema Chimgege.
Nae Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji mpya kata ya
Mnyamani, bw. Rahim Gassi alisema anaishukuru serikali kwa kutembelea mataa
wake kwani maji taka yamekuwa
yakititiririshwa na kusababisha watu kupata magonjwa.
Alisema Maji taka hayo yanayotirirshwa katika mto msimbazi
ndiyo maji yanayomwagiliwa mambogamboga na wakulima kasha kuwauzia watuwatu
hali ambayo si nzuri ki afya.
Post a Comment