Header Ads

Kikosi cha Watu 10,000 chapambana na Moto California, MAREKANI

Zaidi ya wafanyakazi 10,000 wa kikosi cha kuzima moto katika mji wa California wanaendelea kupambana na moto mkubwa katika jimbo hilo.
Maafisa wanasema moto huo mkubwa umesababisha barabara kuu na njia ya reli inayounganisha mji huo na Los Angeles pamoja Las Vegas kufungwa.
Maelfu ya watu wameamuriwa kuondoka katika nyumba zao hata hivyo baadhi wamekataa.
John Miller kutoka kikosi cha huduma za misitu amewataka raia wa nchi kutekeleza amri ya kuondoka.

No comments

Powered by Blogger.