Header Ads

Rais Dkt JOHN MAGUFULI amalizia Uteuzi wa Baraza lake la Mawaziri


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano ya utawala wake.

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

 1.Profesa Jumanne Maghembe - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).

3.    Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Majina Umwagiliaji.

4.    Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri waElimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)

5.    Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6Prof. Makame Mbarawa –Amehamishw a kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwendaWizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.

GersonMsigwa
KaimuMkurugenziwaMawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

No comments

Powered by Blogger.