Header Ads

Makamu wa Rais Mama SAMIA SULUHU ashiriki UHURU DAY kwa Kufanya Usafi na Wananchi wa MOROCCO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kufagia na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 za uhuru wa Tanzania Bara.

Akizungumza na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.

“Haya makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema MHe. Samia.

Alielezea kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.

Makamu wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza  tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa na elimu bora. 

Pamoja na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
  

No comments

Powered by Blogger.