Zoezi la Kugawa Chakula Cha Msaada, Kambi ya Nyarugusu Mkoani KIGOMA Limeendelea
Wakimbizi kutoka nchini Burundi
walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba shehena ya unga wa
mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula hicho Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake
katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
Byesige Josephat (anayemimina
mafuta) na Hezron Mtangirwa (kushoto), wakimbizi kutoka Burundi
waliohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wakipima mafuta
ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana,baada ya kugawiwa mafuta
na Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia chakula (WFP), ambalo
lina kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Kina mama wa kimbizi toka
Burundi wakipata mgao wao wa unga unaotolewa kwa wakimbizi
wanaohifadhiwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma. Serikali kwakushirikiana na Mashirika ya Kimataifa
imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka Burundi wanapata
chakula cha kutosha kwaajili ya mahitaji yao.
Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) wakiwa wamebeba mgao wa chakula.
Wakimbizi wakifunga shehena ya mahindi.
Sehemu ya shehena ya chakula ukiwepo unga wa mahindi na mafuta ya kupikia ikiwa katika ghala la kuhifadhia chakula.
(PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
Post a Comment