Header Ads

WACHINA WAVAMIA JENGO LA MACHINGA COMPLEX, KISA LINADAIWA KUUZWA !!


Jengo la Machinga Complex 
SIRI zimeanza kufichuka ndani ya Manispaa za Jijini la Dar es Salaam,juu ya njama ambazo zinafanywa na watendaji wakubwa wa manispaa hizo za kutaka kuliuza Soko la wafanya Biashara ndogo ndogo la  Machinga Complex liloko Karume jijini dare s salaam, kwa Raia wa kutoka China......Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo.

       Akifichua njama hizo Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Machinga Complex ,Gerald Mpangama leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema Wafanyabiashara wamebaini njama hizo ambazo  wanadai zinasukwa kwa Ustadi mkubwa na Meya wa Jiji Dk Didas Masaburi  pamoja na Watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

“Tunajua fika kuna kitu kilichofichika nyuma nacho ni suala zima la uuzwaji wa Jengo la Wafanyabiashara wadogo wadogo la Machinga Complex kwa watu toka china,kwani hata agenda namba (7)ya kikao cha Bodi kilichopita kilizungumzuia sana suala la uuzwaji wa Jengo hili,”amesema Mpangama.

          Bwana Mpangama ameongeza kuwa mbali na Mstahiki Meya Dk masaburi kuhusika kutaka kuliuza Soko hilo pia yupo Diwani wa Kata ya Upanga Godwin Mbaga ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi na uendeshaji wa jingo hilo.

           Pamoja na hayo Bwana Mpangama  amebainisha kuwa Sababu sababu ambayo Dk Maburi na wenzake wanasema ni kamba soko hilo linajiendesha kuhasara.

       Aidha, Bwana Mpangama amesema kwa sasa wanfanyibiashara hao wamesema hawatakubali soko hilo liluzwe na kusema watafanya Mgomo Mkubwa wa kupinga kuuzwa kwa soko hilo.
   Jengo la Mchinga Complex ambalo limejengwa kwa Fedha za Mkopo kutoka NSSF wa zaidi Bilioni 16 na linatarajiwa kuuzwa kwa Bilioni 86 kwa watu toka Nchini China.

No comments

Powered by Blogger.