Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. .............
Amesema maadili ni nyenzo muhimu sana katika ujenzi wa Taifa na huliepusha kuingia katika mifarakano na migogoro. “Hivyo hatuna budi nasi kuyalinda maadili hayo kwa uwezo wetu wote, ili tuyarithishe kwa vizazi vijavyo, kama vile sisi tulivyoyarithi kutoka kwa waasisi wa Taifa letu,”.
“Hata hivyo, ninyi ni mashahidi kuwa katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia vitendo vya mmomonyoko wa maadili na matokeo yake yanaonekana dhahiri kama kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, kuiga tamaduni za nchi za kigeni ambazo sio njema na hazina tija kwa jamii, na Taifa kwa ujumla”.
“Ni ukweli usiopingika kuwa mmomonyoko wa maadili ni miongoni mwa vichocheo vinavyopelekea matumizi ya dawa haramu za kulevya. Hivyo ni matarajio yangu kuwa mtaliangalia kwa kina tatizo la mmomonyoko wa maadili ambalo kwa kiasi kikubwa linatuathiri kama Taifa katika mipango ya Serikali na maendeleo ya Taifa letu,” amesema.
Hivyo Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa BAKWATA kwa kuwa na wazo la kufanya kongamano hilo lenye kulenga kujadili namna ya kurejesha maadili katika jamii. Tukumbuke kuwa Watanzania tutaendelea kuishi kwa upendo, amani na utulivu iwapo tutazingatia maadili.
|
Post a Comment