Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.
.................................................
TPDC kwa kushirikiana
na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi
asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa
mingine itakayoidhinishwa.
Hayo yamebainishwa na
Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba wakati akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Musomba
amesema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi
wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam,
ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo
yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.
“Napenda kuutaarifu
umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi
asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi
na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.
Aliongeza kuwa lengo
la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha,
mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda
za usambazaji.
Aidha alisema kuwa
ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta
binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa
gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu
utakapomalizika.
Mtandao huo
unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa
kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na
vituo vya kujazia gesi hiyo.
|
Post a Comment