Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa uongozi wa
Kampuni ya ujenzi ya Chicco, wakati alipokuwa akikagua barabara ya Kia-Mererani
yenye urefu wa KM 26, mkoani Arusha, leo.
.............................
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya mchepuo (Arusha bypass)
yenye urefu wa KM 42.4 na kumtaka mkandarasi M/S Hanil Jiangsu J/V anayezijenga
kuhakikisha zinakamilika kwa wakati.
Barabara hizo ambazo
zinajengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 139.34 zina lengo la kupunguza
msongamano wa magari katikati ya jiji la Arusha kwa kuwezesha magari makubwa kupita
nje ya mji.
Aidha, Profesa Mbarawa
amewataka wanachi wa mko wa Arusha kulinda miundombinu yote ya barabara hizo
ili zidumu kwa muda mrefu na kuleta tija inayokusudiwa.
“Tunatumia pesa nyingi
sana kujenga barabara hizi, hivyo nawaomba wananchi tuzilinde na tuzitunze ili
zidumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Profesa. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amewapongeza
wajenzi na wasimamizi wa barabara hizo kwa hatua iliyofikiwa na kuwataka
kuongeza kasi ya ujenzi na kuzingatia thamani ya fedha katika barabara hizo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Arusha Eng. Mgeni Mwanga, amemhakikishia
Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara mkoani Arusha utakamilika kwa
wakati na ubora unaotakiwa.
“Tumejipanga
kuhakikisha barabara ya Sakina-Tengeru na ile ya mchepuo kukamilika kama
ilivyopangwa ili kupunguza msongamano hali itakayovutia ongezeko la watalii na
hivyo kukuza uchumi wa mkoa wa Arusha”, amesema Eng. Mwanga.
|
Post a Comment