Waziri mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara wa kilimo
cha pamba Riyaz Haider wakati wa akitembelea maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi, baada ya mfanyabiashara huyo kupata mkopo kutoka katika benki kuu ya Tanzania kupitia
benki ya NMB.
................................
Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya
Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya
Mafao yanayotolewa na Mfuko huo.
PPF inatoa Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya, unatoa
elimu juu ya mfumo wa ' Wote scheme' kwa sekta isiyo rasmi yaani wale
wanaojiajiri kama vile mama lishe, dereva boda boda, wakulima, wafugaji,
wajasiriamali, Wasanii, wote hawa wanathaminiwa na PPF ndio maana
unatoa fursa za huduma za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na
Mafao ya uzeeni.
Kupitia Maonesho haya PPF inasajili wanachama wapya hapo
hapo viwanjani pamoja na kukabidhi vitambulisho vya uanachama wa Wote
scheme.
Hivyo ni fursa muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika
viwanja vya Maahujaa kupata elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu
ili kufaidika na Wote scheme.
Na kwa wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu nao
Post a Comment