|
Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde akisaini kitabu
cha wageni katika banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi baada ya kupata maelezo ya mpango
wa ‘ Wote scheme’ ambao umekua msaada katika kuwaongezea mitaji vijana kutokana
na mikopo ya mpango huo, waliosimama Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet
Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro
Liganga. | | | |
.........................................
Mfuko wa
Pensheni wa PPF unaendelea kuwakumbusha wananchi kujiunga na PPF ili kuweza
kufaidika na fursa mbalimbali kama vile mikopo ya maendeleo, elimu, huduma ya
afya, mafao ya uzeeni na mafao ya uzazi.
Akiongea
katika Maonesho ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa,
mkoani Dodoma, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel alisema hii ni
fursa pekee kwa waajiriwa wapya wakiwemo walimu, madaktari na kada zingine
kuchagua Mfuko wa Pesheni wa PPF ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya
kimaendeleo.
Afisa huyo
alisema waajiriwa hao wapya wakijiunga na PPF watafaidika na mikopo katika
maeneo yao ya kazi, mafao ya uzazi, mafao elimu, mafao ya ugonjwa, mafao ya
kifo, wategemezi, kiinua mgongo na mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wakati kwa
kutumia kikotoo kilichoboreshwa.
|
Afisa Mwendeshaji wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati Joyce
Rwechungura akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na PPF kwa
waliotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi
kiuchumi inayoendelea katika viwanja vya
Mashujaa mkoni Dodoma. |
|
Mbunge wa
jimbo la Kishetu Mhe. Elias Kwandikwa
akiuliza swali juu mpango wa ‘Wote
scheme’ ulivyofanikiwa kwa watu wote ikiwemo walio kwenye Sekta isiyo rasmi nao
kupata nafasi ya kupata mafao mbalimbali.
Wanaomfuatilia kwa makini ni Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na
Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga. |
|
Katibu wa Chama
cha Wafugaji Tanzania Magembe Makoye akimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa
PPF Astro Liganga kuhusu Mfumo wa ‘Wote
scheme’ ambao kima cha chini cha kuchangia ni shilingi elfu ishirini na ndani
yake kuna fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na
mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo
rasmi kujiwekea akiba.
|
|
Michael Silasi (mwenye miwani ) na
Said Ally (aliyevaa kofia ) wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF
Janet Ezekiel kuhusu kazi za PPF na mafao yanayotolewa na Mfuko
huo ikiwemo mfumo wa 'Wote
scheme' ambao utoa fursa za mikopo ya
maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo huu
unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba. |
|
Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa
Mfawidhi wa PPF Astro Liganga wakitoa maelezo juu ya huduma za PPF kwa Waziri
wa viwanda,biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati alipotembelea Maonesho
ya Mifuko ya uwekezaji kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma. |
Post a Comment