Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yafafanua Hatma ya Ubunge wa Sophia Simba
....................................................
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutarifu Umma kuwa; kwa mujibu wa Kifungu cha 37
(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kuwa; kufuatia Mbunge wa Viti Maalum, SOPHIA MNYAMBI SIMBA kufukuzwa
uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa
Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.
Kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe
katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake
husika cha Siasa.
Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA
amefukuzwa uanachama wa Chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za
kuteuliwa au kugombea Ubunge.
Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya
Ubunge wa Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa
kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Jaji
(R) Semistocles Simon Kaijage
Mwenyekiti
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI
12
Aprili, 2017
Post a Comment