Dkt HAMIS KIGWANGALLA atembelea Kambi ya Wagonjwa wa Kipindupindu Mkoani IRINGA, atoa Maagizo ya Serikali
Eneo la vijiji vya Pawaga linavyoonekana kwa picha za angani wakati wa Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa.
..............................
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangallla amekuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi za juu kufika katika eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Tarafa ya Pawaga iliyopo Iringa vijijini Mkoani hapa ambapo mbali na kutoa pole pia ameweza kutoa huduma za kitabibu kwa baadhi ya watu waliozidiwa waliokuwa bado hawajaokolewa.
Awali Dk. Kigwangalla alipodhuru kwa wananchi waliopo kwenye kambi ya muda baada ya kunusurika na mafuriko hayo, aliwaeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega kwani Serikali ya "Hapa Kazi Tu" haina ngoja ngoja ndio maana yeye ameweza kufika haraka kuakikisha wananchi wapo salama na wanapatiwa huduma zote za msingi na za kijamii ikiwemo matibabu na elimu ya kijikinga na milipuko ya magonjwa ikiwemo magonjwa ya kipindupindu ambacho kimewakumba wananchi hao.
Dk. Kigwangalla ameweza kufanya hilo baada ya Chopa iliyokuwa ikimtembeza angani kufika katika maeneo yaliyozingirwa, alimuru rubani wake kushusha chini na kisha kutoa msaada wa haraka kwa akina mama na watoto waliokuwa wamezingirwa kwenye moja ya maeneo hayo zaidi ya siku tatu bila kuokolewa ambapo alitoa huduma na kisha Chopa hiyo iliwabeba hadi katika eneo maalum waliopo wahanga wengine waliookolewa.
Pia Dk. Kigwangalla aliweza kutoa elimu na maelekezo mbalimbali kwa wahanga hao kujiepusha na masuala ya kutumia mahitaji salama ilikuepukak kipindupindu kisienee zaidi kwani hadi sasa eneo hilo limeweza kupatikana wagonjwa wa ugonjwa huo zaidi ya 220 huku hadi wanatembelea katika kambi ya Mtakatifu Lucas iliyopo Pawaga, ilikuwa na wagonjwa zaidi ya 40.
Imeandaliwa na Magreth Kinabo–MAELEZO, Andrew Chale,Iringa
Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla alipo dhuru kwa kutumia Chopa katika eneo lililokumbwa na mafuriko hayo kijiji cha Mbolimboli.
Baadhi ya wananchi waliookolewa baada ya Naibu Waziri, Dk.Kigwangalla kuamuru wawaishwe katika kambi waliopo wahanga wengine.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipewa maelezo namna wanawake hao pamoja na watoto wao wadogo walivyoweza kuzingirwa na maji kwa muda wa siku tatu bila kuwa na huduma muhimu ambapo hata hivyo, Naibu Waziri aliweza kuwasaidia ikiwemoo kuamuru Chopa hiyo iwapeleke kwenye kambi maalum na kisha wao kubaki hapo kabla ya kurudiwa tena na kuendelea na safari ya Kambi ya watu wa Kipihdupindu.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipata maelezo ya mmoja wa waokoaji wanaotumia boti maalum namna walivyoweza kupata taabu jinsi ya uokoaji katika eneo hilo.
Baadhi ya wahanga wa mafuriko wa vijiji vya Mbolimboli katika Tarafa ya Pawaga wakipata maji maalum yenye dawa ilikujikinga na ugonjwa wa kipindupindu ambao hata hivyo umeenea katika eneo hilo kutokana na maji yake kuchafuliwa na vinyesi vya vyoo vilivyokumbwa na mafuriko.
Naibu Waziri, Dk.Kigwangalla akisisitiza wahanga hao wa mafuriko kuakikisha wanatumia vyakula na vitu vingine kwa hali ya usafi ilikueupuka ugonjwa huo wa kipindupindu.
Baadhi ya akina mama wakipanda Chopa baada ya Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla kuamuru wapelekwe kwenye kambi haraka kutokana na watoto waliokuwa nao kuzidiwa (wanawake hao wanaoonekana pichani ndani ya chopa).
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa wakiwa katika Chopa juu wakiangalia namna mafuriko hayo yalivyosababisha athari kubwa na kufanya kuwa kisiwa katika vijiji hivyo vya Mbolimboli.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akioneshwa moja ya maeneo namna maji yake yalivyochafuliwa na kinyesi baada ya vyoo kuharibiwa na mafuriko hayo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati alipofika katika eneo lililokuwa akina mama hao na watoto ambao wamekaa siku tatu bila kupata huduma muhimu.
Pichani ni baadhi ya akina mama na watoto ambao walikwama kwa zaidi ya si tatu kwenye mafuriko hayo huku wakishindwa kupata mahitaji muhimu ambapo pia vifaa vya uokoaji na waokoaji kushindwa kuwafikia ambapo hata hivyo Naibu Waziri wa Afya. Dk. Kigwangalla alipoamuru Chopa iliyokuwa ikipita kuangalia athari hizo kushuka kisha kuwachunguza na kupelekwa kwenye kambi maalum.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, wakielekea katika kambi ya wahanga hao wa mafurikoeneo la Itunundu..
Baadhi ya watoto wakiwa katika eneo la kambi ya wahanga ambao wengi wao wamekimbia kwenye maeneo hayo yaliyokumbwa na mafuriko.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akisaidiana na mmoja wa watoa huduma baada ya mtoto huyo kuzidiwa katika kambi hiyo maalum.
Post a Comment