Header Ads

BMT yamteua MOHAMMED KIGANJA kuwa Katibu Mtendaji Mpya

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dionis Malinzi wa pili kutoka kushoto akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu uteuzi wa ndugu Said Kiganja kuwa Kaimu Katibu Mtendaji mpya wa Baraza hilo, wa kwanza kulia ni Msemaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Zawadi Msala na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu.(Picha na Benjamin Sawe-WHUSM) 

..........................


BMT IMEMTEUA BWANA MOHAMED KIGANJA KUWA KATIBU MTENDAJI MPYA.

Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limemteua Bwana  Said Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa Baraza hilo kuanzia leo, ili kujanza nafasi ya aliyekuwa Katibu Mtendaji Baraza hilo ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye na kumrudisha Wizarani ili aweze kupangiwa majukumu mengine.

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Sheria iliyoundwa na BMT kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.

Kabla ya uteuzi huo Bwana  Kiganja alikuwa ni Afisa Michezo Mkuu katika ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulipo fanyika.

Pia bwana Kiganja aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Bwana Kiganja ana shahada ya kwanza ya elimu upande wa masuala ya michezo na utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.



Imetolewa na Mwenyekiti wa BMT
Deonis Mallinzi
19/02/2016

No comments

Powered by Blogger.