Rais Dkt JOHN MAGUFULI akutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Mjumbe Maalum wa Rais wa GUINEA BISSAU
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mjumbe Maalum wa
Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau mara baada ya kupokea barua yenye Salamu na
pongezi.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
.........................................................................
Rais wa Jamhuri ya
Guinea Bissau Mheshimiwa Jose' Mario Vaz amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi hiyo itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali, hususani katika uchumi kwa
manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.
Rais Jose' Mario
Vaz amesema hayo katika ujumbe wa barua uliwasilishwa kwa Rais Magufuli na
Mjumbe maalum wa Rais huyo Jenerali Omar Embalo, Ikulu Jijini Dar es salaam leo
tarehe 25 Februari, 2016.
"Napenda
kusisitiza kuwa nchi zetu ni marafiki wa muda mrefu, naomba urafiki na
mahusiano haya mazuri yaendelee na ninakuhakikishia kuwa nchi yangu itaendelea
kuuenzi ushirikiano huu" Ilieleza sehemu ya
ujumbe huo.
Aidha, Rais Jose
Mario Vaz amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Tanzania
katika awamu ya tano na amemualika kuitembelea nchi ya Guinea Bissau ili
kuimarisha zaidi Uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake
Rais Magufuli amemshukuru Rais Jose Mario Vaz kwa kumtuma mjumbe maalum kwa
ajili ya kumletea ujumbe wa pongezi, na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea
kushirikiana na Guinea Bissau.
"Nakushukuru sana Jenerali Umaro Sissoco Embalo
kwa kuniletea ujumbe wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau na nakuomba
umwambie namshukuru kwa pongezi, mimi na serikali yangu tupo tayari kuimarisha
uhusiano na ushirikiano na Guinea Bissau ili mataifa yetu yaweze kunufaika
zaidi"Alisema Rais Magufuli
Wakati huo huo,
Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Ikulu Jijini Dar es salaam
leo.
Gerson
Msigwa,
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
25 Februari,
2016
Post a Comment