Rais Dkt JOHN MAGUFULI afanya Mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt RICHARD SEZIBERA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard
Sezibera Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard
Sezibera Ikulu jijini Dar es Salaam.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo
na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu
Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amepokea
taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki utakaofanyika tarehe 02 Machi, 2016 Katika Jiji la Arusha, Nchini
Tanzania.
Rais Magufuli
ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi tano
wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Akizungumza mara
baada ya mazungumzo hayo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera,
amesema maandalizi kuhusiana na mkutano huo yanakwenda vizuri.
Amesema pamoja na
mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo mpango wa kuanzisha
viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza uingizaji wa magari kutoka
nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Kuhusu hali ya
Jumuiya, Dkt. Sezibera amesema inaendelea vizuri na ametaja baadhi ya mambo
ambayo yamefanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa umoja wa forodha, makubaliano
ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu moja.
Mengine ni kuwepo
kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile reli na umeme ndani
ya Jumuiya, na mazungumzo kuhusu umoja
wa kisiasa.
Kwa upande wake Waziri
wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt.
Augustine Mahiga, amesema Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa kikao hicho ipo tayari
kupokea ugeni na kwamba pamoja na kufanyika kwa kikao hicho, marais wa Tanzania
na Kenya watafungua barabara inayounganisha Tanzania na Kenya katika Mpaka wa
Holili na kutakuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha pamoja
cha mpakani kwa ajili ya kuwezesha upitaji wa mizigo na watu yaani "One
Stop Boarder Post"
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es
salaam
24
Februari, 2016
Post a Comment