Header Ads

Jamii imeshauriwa Kutumia Mfumo wa Unenepeshaji wa Mifugo ili Kuzalisha Nyama yenye Ubora

Mkurugenzi Msaidizi uendelezaji wa miundombinu ya mifugo na masoko Bw. Aaron Luziba kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu  unenepeshaji wa mifugo amabo mifugo kabla ya kuuzwa huwekwa kwa pamoja kwa siku 90 hadi 120 na kuwalisha vyakula vyenye wanga na protini ili kuzalisha nyama zenye ubora ikiwemo ladha nzuri na laini, Wakati wa mkutano leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Daktari mkuu wa Mifugo Bw. Sero Luwongo.
Daktari mkuu wa Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Sero Luwongo akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa wafanyabiashara umuhimu kuwaona maafisa ushauri wa mifugo kabla ya kupeleka mifugo kwenye mauzo ikiwa ni pamoja na kubaini magonjwa ili kuwawezesha kuuza mifugo yenye afya na matunzo mazuri, Wakati wa mkutano leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi uendelezaji wa miundombinu ya mifugo na masoko Bw. Aaron Luziba.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments

Powered by Blogger.