Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa
Kikao cha Siku moja kilichowashirikisha Viongozi wa Mradi huo kutoka JICA pamoja na wahandisi wa
Halmashauri ambazo mradi huo unatekelezwa ukilenga kuboresha miundo mbinu
katika Halmashauri hapa nchini.
Frank Mvungi-MAELEZO
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Mussa Iyombe amewataka
wananchi kutunza barabara zinazojengwa
na Serikali kwa kushirikiana na wafadhili katika Halmashauri zote hapa
nchini.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika hafla
fupi ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi na ukarabati wa
barabara za halmashauri nchini Iyombi
amebainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa
na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .
“Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri za Iringa,Mufindi,Chamwino na Kondoa”
alisisitiza Iyombe.
Akifafanunua kuhusu utekelezaji wa mradi huo Iyombe amebainisha kuwa unadhamiria kujenga uwezo kwa wahandisi wa
Mikoa na Halmashauri hapa nchini ili
waweze kushirikiana na wananchi katika kujenga
na kulinda miundo mbinu hiyo kwa maslahi ya Taifa.
Aidha Iyombi
amewata wakurugenzi wa Halmashauri ambazo mradi huo unatekelezwa kutunza barabara hizo ili zilete matokeo
yaliyokusudiwa.
Akizungumzia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Japan
na Tanzania Iyombe amesema kuwa maeneo ambayo Tanzania imekuwa ikipata ufadhili
kutoka Japan ni Sekta ya Kilimo,Viwanda,Uimarishaji wa Utawala bora.
Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa Shirika la
Maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na
Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa barabara katika
Halmashauri hapa nchini unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza
imekamilika katika Halmashauri za Chamwino na Iringa na awamu ya pili
imekamilika katika Halmashauri za Kondoa na Mufindi ambazo ripoti ya
utekelezaji wake iliwasilishwa leo katika mkutano wa siku moja ulifanyika
Jijini Dar es salaam ukilenga kufanya tathmini ya utekelezaji kabla ya kuanza
kwa awamu ya tatu.
|
Post a Comment