Header Ads

Ziara ya Naibu Waziri wa Nishati yasimamisha Kazi Mameneja wawili

 Na Zuena Msuya, Dar es salaam

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani  amewataka wandarasi wanaotekeleza mradi mkubwa wa umeme wa TEDAP kwa jiji la Dar Es salaam kumaliza mradi huo mwishoni mwa Mwezi wa Septemba ili jiji hilo liwe na umeme wa kutosha na wa uhakika na kuwasimamisha kazi Mameneja Wawili wa kituo cha kupooza umeme cha Kurasini.

Dkt.Kalemani ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kushtukiza ya kukagua vituo vitano vya kupooza umeme pamoja na njia kuu ya kusafirisha umeme wa msogo wa 132Kv ulioanza kujengwa mwaka 2012 na ulitarajiwa kukamilika mwaka 2013.

Dkt.Kalemani alisema kuwa mradi huo umelenga kuimarisha upatikanaji wa umeme katika jijini la Dar es salaam kutokana na kuwepo kwa mahitaji makubwa ya umeme katika viwanda, sehemu za biashara , huduma za kijamii pamoja na makazi ya watu.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani( katikati) akitoa maagizo kwa Msimamizi Mkuu wa mradi wa Tedap, Mhandisi Emmanuel Manirabona(kulia) katika moja ya vituo vya kupooza Umeme wa msongo wa 132 kV ili kupata umeme wa kutosha na wa uhakika kwa jiji la Dar es Salaam.

Alifafanua kuwa Serikali haiwezi kufanya kazi na mikataba ya wakandasi isiyokwisha kwa wakati, hivyo aliwaagiza Tanesco kuangalia upya mikataba ya wakandasi wote nchini wanaotekeleza miradi ya umeme kama kuna mikataba ilioisha uhuishwe na kama haihitajiki ufutwe .

"mradi huu ulianza 2012 na ulitakiwa kukamiliaka  2013 yaan ndani ya miezi 18 na mpaka sasa ni zaidi ya miaka nne hii haikubaliki hata kidogo hatuwezi kuwa na miradi isiyokwisha", alisema Dkt Kalemani.

Katika ziara hiyo, Dkt Kalemali aliwasimamisha kazi Maneneja wawili wa kituo cha kupooza umeme cha Kurasini kwa kosa la kutosimamia ipasavyo majukumu yao na kumuagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi huo wa Tedap, Emmanuel Manirabona  kuweka Mameneja wapya katika kituo hicho.
Moja ya msingi wa kusimamisha nguzo za njia kuu ya kusafirisha umeme wa msongo wa 132kV kwa mradi wa umeme wa Tedap kwa jiji la Dar es salam.
Moja ya nguzo za njia kuu ya kusafirisha umeme wa msongo wa 132Kv kwa mradi wa umeme wa Tedap kwa Jiji la Dar es salam ukiwa chini kabla ya kusimikwa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(kushoto) akizungumza na baadhi ya vibarua wanaosimika nguzo za kusafirisha njia ya umeme wa 132kV kwa Jiji la Dar es salaam ili kupata umeme wa kutosha na wa uhakika. 

Akizungumzia ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme, Dkt Kalemani alisema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2012 na ulitarajiwa kukalika mwaka 2013 lakni mpaka sasa kituo hicho cha Kurasini kimetekeleza mradi huo kwa asilimia 50 ya ujenzi wa mradi huo tofauti na vituo vingine.

" Dar es salaam inahitaji umeme wa uhakika ,nimefanya ziara ya kushtukiza kujua mradi huu unaendeleaje ,nilikuja hapa februari kazi haikuwa ikifanyika mpaka sasa  vilivile hatuwezi kufanya kazi namna hiyo', alisisitiza Dkt. Kalemani.

Aidha aliongeza kuwa katika vituo vya kupoza umeme vya Gongolamboto, Mbagala, na Kipawa kazi kubwa iliyobaki ni kuvuta nyaya na kunganishwa katika njia kuu ya umeme  hivyo wakandarasi hayo wahakikishe wanamaliza kazi hiyo kwa wakati.

Katika hatua nyingine Dkt Kalemani alitoa rai kwa wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) nchi nzima kutoka maofini na kufuata wateja ili kuwapatia huduma.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi  wa Tanesco wamekuwa wakikaa maofisini bila kufahamu mahijati ya wateja wao na hivyo kuwapa wakati mgumu wateja pale wanapohitaji huma hizo kwa karibu.

Vituo vitakavyotumika kupooza umeme wa mradi wa  Tedap ili kupata umeme wa kutosha na wa uhakika kwa jiji la Dar Es salaam ni pamoja na Kurasini, Mbagala, Gongolamboto, Kipawa na Ubungo. 

No comments

Powered by Blogger.