Na Mathias Canal, Dodoma
Watanzania wametakiwa kuthamini na kununua bidhaa zinazozalishwa nchini
Tanzania hususani katika sekta ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi kwani hakuna sababu
ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi ilihali bidhaa hizo wanazoagiza
zinazalishwa na watanzania wenzao.
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said ameyasema hayo mara
baada ya kutembelea baadhi ya mabanda katika maonyesho ya wakulima Nane nane
Kanda ya kati Dodoma yanayofanyika katika uwanja wa Nzuguni huku kauli mbiu ya
mwaka huu ikiwa ni "Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni nguzo ya maendeleo, Kijana
shiriki kikamilifu (Hapa Kazi Tu).
Jaffo amesema kuwa asilimia kubwa
ya watanzania wamekuwa watumwa wa mambo ya kigeni, kuiga tamaduni mbalimbali
ikiwemo matumizi ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi wakati pia bidhaa hizo
zinazalishwa nchini, huku akitolea mfano wa manunuzi ya viatu kutoka nchi
mbalimbali wakati hapa nchini Jeshi la Magereza linatengeneza viatu bora vya
ngozi tena kwa bei nafuu.
|
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisalimiana
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne
Mtaturu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa maonesho ya nane nane
Nzuguni mjini Dodoma.
|
|
Naibu
waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza kwa
makini maelezo ya kilimo cha
mbogamboga yanayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa JKT. Sambamba na hayo pia Naibu Waziri huyo ameiagiza Mamlaka ya Ustawishaji
Makao makuu Dodoma kusimamia vyema na kwenda na kasi kubwa katika utengenezaji
wa stendi kubwa na ya kisasa ili kufanana na mji wa Dodoma ambapo pia hivi
karibuni makao makuu ya serikali yatahamia mjini hapo.
Aidha ameongeza kuwa Maonesho hayo yanapaswa kuboreshwa ili maonyesho yajayo
yawe ya kitaifa ambapo nchi mbalimbali zitapata fursa ya kutembelea na kuifanya
Tanzania kujikomboa katika wimbi la umasikini.
Maonesho hayo yanahusisha Shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji
wa nyuki, wavuvi, wana mazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na
mifugo, wizara taasisi/Makampuni ya umma, makampuni Binafsi, mabenki, taasisi
za umma na za binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali. |
|
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza
kwa makini maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyeji wake katika Maonesho hayo
ambaye ni mkuu wa Wilaya ya ikungi
Miraji Jumanne Mtaturu.
|
|
Naibu
waziri TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisaini
kitabu cha wageni katika banda la Mwanzo
Bora Nutrition Program. Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya waandaaji wa Maonesho hayo Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji
Jumanne Mtaturu amesema kuwa maandalizi ya maonyesho hayo yametumia muda
mfupi lakini kwa kiasi kikubwa yamekuwa bora na kuahidi kuwa na Maonesho yajayo
kuwa bora zaidi katika kipindi kinachokuja.
Mtaturu amesema kuwa lengo mahususi la maonesho hayo ni utoaji wa elimu ya
matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi ambapo
watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali.
Ameongeza kuwa maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye
tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa ili kuongeza thamani.
Dc Mtaturu amesema kuwa pia wadau
watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, Mashirika ya umma na
binafsi, ambapo wafanya biashara wanayatumia maonesho hayo kwa kuuza bidhaa,
kufahamiana na kuingia makubaliano. |
|
Naibu
waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Jafo Suleiman Said akisikiliza maelezo
ya namna ya kulima kilimo na ufugaji wa kisasa. Kwa upande wake Katibu wa maandalizi ya Maonesho hayo Aziza Rajabu Mumba amesema kuwa Wanatarajia kila mwananchi
atakayetembelea maonesho hayo kwenda kutekeleza kwa vitendo anayojifunza katika
eneo lake na kuwafundisha wengine ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria kwenye
Maonesho hayo.
Aidha amesema Malengo ya muda mrefu ni kuendeleza uwanja wa Nzuguni ufikie
ubora na hadhi ya viwanja vya maonesho ya Kilimo Kimataifa na kuendelea
kushawishi wadau mbalimbali kuwekeza ili kuufanya uwanja wa Nzuguni uwe kituo
cha huduma cha Maonesho ya Kilimo nchini kama ilivyo kwa uwanja wa Mwalimu
Nyerere Dar es salaam kwa maonesho ya Biashara. |
Post a Comment