Header Ads

Wizara ya Afya yatoa Tathmini Kuhusu Hali ya Kipindupindu Nchini

Waziri wa Afya, UMMY MWALIMU



TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 9 MEI,  2016.


Ndugu wanahabari,

Serikali kupitia Wizara yangu inaendelea na utaratibu wa kutoa taarifa ya mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini kila wiki kama tulivyoahidi. Takwimu za ugonjwa huu zinaonyesha kuwa hadi kufikia tarehe 08 Mei 2016, kulikuwa na jumla ya wagonjwa 21,262  ambao wametolewa taarifa ya kuwa na ugonjwa huu, na kati ya hao, watu 333 wamepoteza maisha.

Katika kipindi cha mwezi mmoja yaani mwezi wa Aprili 2016, idadi ya wagonjwa imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa lakini katika kipindi cha mwezi Mei, 2016 kasi ya maambukizi imeanza tena kuongezeka.
. Takwimu za wiki iliyopita kuanzia tarehe 2 hadi 8 Mei 2016 zinaonyesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa kipindupindu imeongezeka, ambapo idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa ni 138 na vifo 2, ikilinganishwa na wagonjwa wapya 104 walioripotiwa wiki iliyotangulia, sawa na ongezeko la 32%Takwimu hizi ni zinaonesha kuwa juhudi zaidi ziahitajika katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.

Mikoa ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wiki hii ni Kilimanjaro (58, kifo 1), Dar es Salaam (29) na Morogoro (22, kifo 1), Pwani (16) na Mara (15). Halmashauri zilizoongoza kutoa wagonjwa wengi ni Same), Kinondoni, Mvomero), Mbulu, Tarime vijijini, Ilala, Tarime mjini, Temeke, Morogoro vijijini  Kilolo  Morogoro mjini, Bagamoyo, Kisarawe.

Katika wiki iliyopita, mikoa ambayo haikuwa na wagonjwa wa kipindupindu ni Kigoma, Dodoma, Mwanza, Geita, Singida, Shinyanga, Arusha, Tanga, Tabora, Lindi, Kagera, Rukwa, Katavi, Mbeya, Simiyu na Mtwara.


Ndugu wanahabari,
Kama nilivyoeleza hapo juu, takwimu zinaonyesha kuwa ugonjwa unaongezeka, hivyo tunahitaji kuchukua tahadhari kubwa, hususan wakati wa huu wa mvua, ambapo kuna uwezekano mkubwa wa maji ya mvua kusambaza vimelea vya ugonjwa huu. Tujitahidi kuzuia maambukizi, na pia kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa kila siku, hata kama hakuna wagonjwa, na kusimamia kikamilifu hatua mbalimbali za udhibiti wa mlipuko huo.

Ndugu wanahabari,

Wizara inaendelea kutoa rai kwa wananchi wote kuzingatia kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira. Aidha wananchi  wanashauriwa kutumia maji safi na salama na hii ni pamoja na kuhakikisha maji ya kunywa yanachemshwa au kutibiwa kwa dawa kama maagizo ya wataalam yanavyoelekeza. Napenda pia kusisitiza kwa wananchi wanaokaa kandokando ya Mto Pangani hususani mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, kuwa maji ya mto huo si salama, kwa kuwa yamechafuliwa na vimelea vya kipindupindu. Ni muhimu sana kuyachemsha au kuyatibu kwa dawa maji hayo kabla ya kuyatumia nyumbani. Napenda kusisitiza tena    kwamba n marufuku   kw watu   kutitirisha   maj tak ovyo, hasa katika kipindi hiki cha mvua na  mamlaka husika zinatakiwa kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote watakaokiuka agizo hili. Aidha tunawasihi viongozi mbalimbali wa ngazi zote; za vitongoji, vijiji, kata na tarafa kusimamia kikamilifu suala hili, hususan wakati huu wa mvua za masika

Ndugu wanahabari,
Tunaendelea kuisihi jamii kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia yafuatayo:
§  Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo tunamoishi ili kupunguza hatari ya kuenea kwa ugonjwa huu.
§  Kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo na baada ya kumsafisha motto aliyejisaidia.
§  Mamlaka za maji zilizopo nchini zihakikishe upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
§  Kuzingatia ushauri na elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, ili jamii iondokane na imani potofu kuhusu kipindupindu. Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu,
§  .
§  Kufikisha wagonjwa wa Kipindupindu mapema katika vituo vya kutolea huduma ili wawahi kupata matibabu.
§  Kuzingatia matumizi sahihi ya ORS kwa wagonjwa walioanza kuonesha dalili ili kupunguza athari za ugonjwa.
§  Watumishi wa afya kutoa takwimu sahihi na kamili za ugonjwa kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Wizara.


Hitimisho

Wizara inawapongeza na kuwashukuru wadau wote kwa jitihada za dhati zinazoendelea kutekelezwa na katika kusimamia kikamilifu  miongozo inayotolewa na Wizara ili kuutokomeza ugonjwa huu, wakiwemo wataalamu wa sekta mbalimbali, Mashirika ya Kimataifa, Watumishi, Mikoa na Halmashauri pamoja na waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla.



Asanteni sana

No comments

Powered by Blogger.