Header Ads

Mazungumzo Kuhusu Mzozo wa SUDAN sasa Kufanyika ETHIOPIA


Pande zinazozozana nchini Sudan Kusini zinatarajiwa kufanya mazungumzo zaidi nchini Ethiopia hivi leo.

Itakuwa siku ya mwisho ya mazungumzo ya amani kabla ya vikwazo vya kimataifa kuwekewa pande zote.

Lakini serikali ya Sudan Kusini pamoja na waasi wamesema huenda wakahitaji muda zaidi kutatua maswala kama vile ugavi wa madaraka katika serikali ya mpito.

Mwakilishi maalum wa Muungano wa Ulaya, Alexander Rondo, ameonya kuwa ucheleweshwaji wa kufikia makubaliano hautavumiliwa.

Wapiganaji wa Sudan

Marais wa Uganda, Kenya na Ethiopia pia wanashiriki mazungumzo hayo. Jitihada za awali za kujaribu kutatua mzozo huo zimeshindwa.

No comments

Powered by Blogger.