Header Ads

Mabondia Kupima Uzito Ijumaa, Kuzichapa Jumamosi Shule ya Uhuru Wasichana

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Ally Mulo watapima uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya mpambano wao wa
jumamosi utakaofanyika katika viwanja vya basketball vilivyopo katika shule ya uhuru wasichana Kariakoo Dar es salaam.

Akizungumzia mpambano huo mratibu ambaye pia ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema mabondia hawo watapima uzito siku ya ijumaa sdaa tatu asubui kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi agost 22.

Mbali na mabondia hawo mabondia wengine watakao oneshana kazi siku hiyo ni kelvin Majiba atakaepambana na Vicent Mbilinyi wakati Husein Pendeza akioneshana umwamba na Shomari Mirundi na Raymond Mbwago atazidunda na Roger Masawe na mapambano mengine mengi ya mabondia chipkizi

Mabondia hawo watapima uzito katika tawi la mashabiki wa yanga bomba lililopo mtaa wa ndanda Kariakoo na mpambano wao kufanyika siku ya jumamosi kuanzia saa kumi na mwisho kabisa itakuwa saa kumi na mbili jioni ili kila mtu afurahie ngimi izo zitakazochezwa mapema na kumalizika mapema kabisa katika siku hiyo

No comments

Powered by Blogger.