Header Ads

CCM yatangaza Kamati ya Kampeni Kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2015

NA
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari jioni hii katika ofisi ndogo ya Makao makuu CCM Lumumba wakati alipotangaza Kamati maalum ya Kampeni za uchaguzi mkuu ujao zinazotarajiawa kuzinduliwa Agosti 23 mwaka huu.

NA2
Baadhi ya wapiga picha wa Televisheni na magazeti  kutoka vyombo mbalimbali wakipata picha wakati Katibu Mwenezi huyo alipokuwa akitangaza kamati hiyo.
………………………………………………………………………

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-

KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
  1. Ndugu Abdulrahman Kinana –        Mwenyekiti
  2. Ndugu Rajab Luhwavi –        Makamu Mwenyekiti – Bara
  3. Ndugu Vuai Ali Vuai           –        Makamu Mwenyekiti – Z’bar
  4. Ndugu Sofia Simba
  5. Ndugu Mohamed Seif Khatib
  6. Ndugu Asha-Rose Migiro
  7. Ndugu Samwel Sitta
  8. Ndugu Nape Nnauye
  9. Ndugu Mwigulu Nchemba
  10. Ndugu Harrison Mwakyembe
  11. Ndugu January Makamba
  12. Ndugu Amina Makillagi
  13. Ndugu Christopher Ole Sendeka
  14. Ndugu Stephen Wasira
  15. Ndugu Abdallah Bulembo
  16. Ndugu Hadija Aboud
  17. Ndugu Mohamed Aboud
  18. Ndugu Lazaro Nyalandu
  19. Ndugu Issa Haji Ussi
  20. Ndugu Waride Bakari Jabu
  21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
  22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
  23. Ndugu Maua Daftari
  24. Ndugu Stephen Masele
  25. Ndugu Pindi Chana
  26. Ndugu Shaka Shaka
  27. Ndugu Makongoro Nyerere
  28. Ndugu Bernard Membe
  29. Ndugu Sadifa Juma Khamis
  30. Ndugu Antony Diallo
  31. Ndugu Livingston Lusinde 
  32. Ndugu Ummy Mwalimu 
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
18/08/2015

No comments

Powered by Blogger.