Header Ads

BASATA yaifungulia Kampuni ya LINO, Mashindano ya Miss Tanzania Kurejea tena !

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lino International Agency Hashim Lundenga,akizungumzia kurejeshewa haki ya shindano la Miss Tanzania.

  Hashim Lundenga, Mkurugenzi wa Lino International.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa Geofrey Mngerteza akizungumza na waandishi wa habari, hawapo pichani.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa Geofrey Mngereza akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Lino International Agency Hashim Lundenga.

Na Mwandishi wetu


Baraza la sanaa taifa (BASATA) limetangaza kulifungulia shindano la urembo la  Miss Tanzania baada ya waandaji wa mashindano kampuni  ya Lino international Agency kurekebisha baadhi ya kasoro zilizojitokeza.

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mtendaji wa baraza la sanaa Taifa Geofrey Mngereza amesema baraza limeamua kuyafungulia mashindano hayo kufuatia waandaji kuomba radhi pamoja na kutekeleza baadhi ya kanuni na taratibu za uendeshaji wa mashinado hayo ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakalam wa ngazi zote za mashindanio.

Aidha mngereza amesema kuwa baraza wameipa miezi minne ya uwangalizi kwa waaandaji wa mshindano kuangalia kama watamaliza baadhi ya changamoto zilizo

kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Lino international agency Hashimu Lundenga amesema kwa sasa kampuni hiyo imejapanga vya kutosha kuhakikisha inakabiliana na changamoto zilizojotokeza awali hazijiludii tena.

No comments

Powered by Blogger.