Header Ads

EDWARD LOWASSA AREJESHA FOMU YA URAIS MAKAO MAKUU YA CHADEMA

 WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, akipungia wafuasi wa CHADEMA na wananchi wengine waliofurika makao makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi Agosti 1, 2015, baada ya kurejesha fomu za kukiomba chama chake kumteua kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ndiye atakayesimama kwa niaba ya vugucugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Na Mwandishi wetu
 
WAZIRI Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, ambaye leo Jumamosi Agosti 1, 2015 amerejesha fomu za kuomba chama chake kipya cha CHADEMA, kimteue kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya vyama vinavyounda vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi maarufu kama UKAWA, ameanza na mtaji wa “kura”  zaidi ya Milioni 1.6, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, mafunzo na msimamizi wa Kanda 10 za chama hicho, Benson Kigaila ametangaza.
 
Kigaila amesema, idadi hiyo ni ya wanachama wa CHADEMA na wananchi wengine ambao wamemdhamini katika fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama hicho. 
 
“Wote waliomdhamini, kwakuwa walikuwa wengi nchi nzima, tulitoa masharti kuwa kila anayetaka kufanya hivyo awe na kadi ya kupigia kura na aweke namba yake ya simu ya mkononi na wote wamefanya hivyo na hii ina maana kuwa CHADEMA, chini ya UKAWA, tuna kura za Rais milioni 1,662, 397.” Alifafanua Kigaila, wakati akielezea utaratibu uliotumika wa wana CHADEMA kumdhamini Mh. Lowassa.
 
Hatua hiyo ya Mh. Lowassa, ya kurejesha fomu zilizopokelewa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Profesa Abdallah Safari, inasubiri hatua nyingine ya Kamati Kuu ya chama hicho ambayo inakutana Agosti 2, 2015 ili kuzipitia fomu hizo kuona kama zinakidhi matwaka ya kikatiba na kanuni za chama hicho kabla ya kupelekwa kwenye vikao vingine vya juu na hatimaye kwenye mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 4, 2015 hapa jijini Dar es Salaam.
 
 Wafuasi wa CHADEMA, wakimshangilia Mh. Lowassa, alipokuwa kitoka kwenye makao makuu ya chama hicho baada ya kurejesha fomu.
 
 Mh. Lowassa, akikabidhi fomu hizo, kwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Tanzania Bara), Profesa Abdallah Safari.
 
 Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Kanda 10 za CHADEMA, Benson Kigaila, akionyesha lundo la fomu zilizomdhamini Mh. Lowassa.
 
 Mh. Lowassa, akipongezwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya chama hicho, Mabere Nyaucho Marando.
 
 Wabunge wa CHADEMA na majimbo yao kwenye mabano kutoka kushoto, Godbless Lema (Arusha Mjini), Wenje (Nyamagana), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).
 
 Mh. Lowassa, akiwasili makao makuu ya CHADEMA.
 
 Mh. Lowassa, akiwa na Esther Bulaya.
 
 Profesa Safari.
 
 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, (Zanzibar), Salum Mwalimu.
 
 Mtoto wa mwisho wa Mh. Lowassa, (katikati), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa CHADEMA, wakati baba yake Mh. Lowassa aliporejesha fomu.
 
 Wabunge na viongozi wa CHADEMA.
 
 Vijana wa 4U ambao walimuunga mkono Mh. Lowassa wakati akiwa CCM, na sasa wanaendelea kumuunga mkono akiwa CHADEMA.
 
 Wananchi waliofurika makao makuu ya CHADEMA wakati Mh. Lowassa akirejhesha fomu.
 
 Mh. Lowassa, akiteta jambo na Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene.

No comments

Powered by Blogger.