Header Ads

TUNATAKA BAJETI YENYE MRENGO WA KIJINSIA-TGNP


Pichani ni Mkurugenzi wa TNGP Mtandao Be Liundi akizungumza na waandishi wa Habarikwenye Semina iliyoandaliwa na TNGP
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema kuwa hautakuwa tayari kuunga mkono watia nia au chama chochote cha siasa ambacho katika sera zake hakitaonyesha mrengo wa kijinsia katika kutetea haki za wanawake,watoto, Walemavu na vijana.Anaandika .

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji TGNP,Lilian Liundi wakati wa warsha ya siku mbili ya waaandishi wa habari iliyolenga kujenga uelewa wa pamoja kuhusu dhana ya kijinsia.


      Amesema, kuwa ni vema vyama vya siasa vikaweka uwiano sawa katika rasilimali zinatumika kutangaza nia ili kuwapa fursa wanawake walionauwezo wa kuongoza na hawana rasilimali za kutosha kutangaza nia.


      Ameongeza, kuwa TGNP aitakuwa tayari kuwaunga mkono wanasiasa ambao hawataonyesha nia ya kutatua matatizo ya kijinsia.


"Tunataka watamke rasmi kwamba nafasi moja wapo kati ya  3 za juu kwa watakao shika madaraka zichukuliwe na wanawake....namaanisha Waziri mkuu,Makamu wa Rais au Rais awe mwanamke,"alisema Liundi


Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Semina ya TNGP

     Aidha amesema katika masuala ya bajeti,kila Wizara husika zitamke wazi uwiano wa kijinsia katika makundi husika pamoja na kutaja fungu lilotengwa kwa kila kundi.


     Kwaupande wake Mkurugenzi wa Bodi ya TGNP, Vicencia Shule amesema kuwa wanachi wanatakiwa kuwa makini kwani viongozi wengi wamekuwa wakitumia rasilimali kubwa katika mambo yao ya kisiasa kuliko kusaidia huduma za kijamii.


Hata hivyo ametoa rai kwa wanawake waliopata nyadhafa za juu na kupata bahati ya kuingia katika mabaraza ya bajeti,kuyapa kipaumbele makundi maalum ili kuwakomboa wanawake walio nyuma yao.

No comments

Powered by Blogger.