Header Ads

ASKOFU CHARLES GADI WA HUDUMA YA GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY AFANYA MAOMBI NCHINI INDIA

 
 Askofu Charles Gadi  wa Huduma ya Good News for all Ministry akiwa katika matukio tofauti wakati akifanya maombi makubwa katika mji wa Hydrabad nchini India ili joto lipungue kwani tayari limekwisha uwa watu 2500 kutoka na kupanda hadi kufikia kiwango cha joto centgrade 50.
 Maombi yakiendelea.

Na Dotto Mwaibale

ASKOFU Charles Gadi  wa Huduma ya Good News for all Ministry akifanya maombi makubwa katika mji wa Hydrabad nchini India ili joto lipungue kwani tayari limekwisha uwa watu 2500 kutoka na kupanda hadi kufikia kiwango cha joto centgrade 50.

Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu toka nchini humo alisema hali hiyo imetokana na maeneo kadhaa ya nchi hiyo kuwa na wimbi kubwa la upepo wa joto (heat wave) na kusababisha vifo hivyo.

"Habari hii kwetu si njema ndio maana nimeamua kuja kufanya maombi haya makubwa nchini humu na wenzangu kwani linatokana uharibifu wa mazingira ambapo hata huko nyumbani linaweza kutokea" alisema Askofu Badi.

Alisema watu waliokufa ni wengi, wazee, watoto na maskini ambao hawana uwezo wa kujikinga na wimbi hilo la joto kwani unahitaji uwe na viyoyozi 'Air conditioning' au maji baridi ya kujinyunyuzia wakati wimbi hilo la joto likipita.

Kutokana na hali hiyo sisi kama viongozi wa kiroho tumesukumwa na mungu kuja nchini humu kufanya maombi haya tukiamini mungu atatusaidia atukinge na joto hilo linalosababishwa na uharibifu wa mazingira.

Alisema maombi hayo yataambatana na utoaji wa misaada kwa waathiriwa wa joto hilo.  

No comments

Powered by Blogger.