Watanzania Watakiwa Kujali Afya zao Kwa Kupima Mara kwa Mara
Katika ni Robert Paul ambae ni Meneja Masoko ya Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO Kanda ya Ziwa, akizungumza katika zoezi la Utoaji bure wa huduma mbalimbali za Afya ikiwemo upimaji wa Magonjwa ya Moyo, Utoaji wa Matibabu kwenye majeraha(Vidonda) pamoja na Uchangiaji damu lililofanyika juzi jumamosi February 06,2016 katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
......................
"Tigo tumeamua kushiriki zoezi hili ili kuonyesha mfano katika jamii namna tunavyojumuika na Watanzania katika shughuli za Kijamii, hivyo kupitia fursa hii ningependa kuwaasa Watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ikiwemo kupima shinikizo la damu, saratani lakini kubwa zaidi kuwa na moyo wa kujitolea kuchangia damu ili kuwasaidia wenye uhitaji wa damu. Alisema Paul.
Nae Cassim Aziz (Kushoto) ambae ni Meneja Masoko wa Tigo Mkoani Mwanza, alizishauri taasisi pamoja na makampuni mbalimbali nchini kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii hususani kuhamasisha watanzania kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka athari za kiafya zinazoweza kuzuilika.
Zoezi hilo liliandaliwa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Udaktari Hubert Kairuki cha Jijini Dar es salaam wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kuenzi Miaka 17 tangu mwasisi wa chuo hicho afariki dunia (Februa 06,1999) ikiwa ni miaka miwili baada ya kuanzisha chuo hicho.
Dkt.Emmanuel Chacha ambae ni Mkurugenzi wa Hospital ya CJ Jijini Mwanza akizungumza katika shughuli hiyo ya upimaji wa afya bure ambapo Hospital ya CF ilikuwa miongoni mwa wadau waliofanikisha shughulio hiyo.
Mwenye Kinasa Sauti ni Dkt.Francis Tegete ambae ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Profesa Paschalis Rugarabamu ambae ni Mlezi wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Picha ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Wadau waliofanikisha zoezi la Upimaji afya bure wakiwa katika Picha ya Pamoja ya wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Hubert Kariuki wanaofanya kazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, akizungumza katika shughuli hiyo.
Kampuni ya Mawasiliano Tigo ikiendelea na Utoaji wa Huduma zake za Simu kwa wateja.
Mmoja wa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo akipatiwa huduma na wahudumu wa Kampuni hiyo.
Wanafunzi na Wananchi mbalimbali walijitokeza kupima bure afya zao.
Zoezi la Upimaji na utoaji huduma za afya bure likiwa linaendelea.
Bank ya Damu salama Kanda ya Ziwa ikiendelea na zoezi la ukusanyaji damu kutoka kwa wananchi waliokuwa wanajitolea damu.
Katikati ni Alfredy Chibuae ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Taaisi ya Tanzania Rural Health Movement akifuatilia utoaji wa huduma unavyoendelea. Taasisi hiyo inashughulika na utoaji wa huduma za afya bure kwa watu wasiojiweza hususani watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (mitaani) pamoja na utoaji wa huduma za dharura ikiwemo wale wanaopata ajali. Taasisi hiyo inapatikana Bugando Jijini Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi
Post a Comment