Picha mbalimbali zikimuonesha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akitoa taarifa ya uteuzi wa uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Katika uteuzi huo Rais Magufuli amewateua mabalozi watatu,
Makamishna wa Polisi wanne na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA)
Picha na IKULU
.............................................
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi
watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa.
Rais Magufuli pia
amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.
Vituo vya
uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia
kukamilika.
Kwa upande wa
Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
1.
Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa
cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es salaam. Kamishna Sirro
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
2. Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa
cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na
Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve
aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
3.
Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Intelijensia. Kamishna Mikomangwa
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
4. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi Nsato Marijani Mssanzya
ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara
ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna
Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses
Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya
Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika
Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Teuzi zote
zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
15
Februari, 2016
|
Post a Comment