NHIF yatumia Mtandao wa Simu Kuwasilisha Taarifa za Mama Mjamzito na Watoto Wachanga
Afisa Mradi wa KFW kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Francis Mbwana akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya Afya mkoani Tanga iliyofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa.
Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga, Dinna Mlwilo akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.
Watoa huduma za afya ya mama na mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani Tanga wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watoa huduma wa Afya ya Mama na Mtoto,uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa Tanga.
…………………………………
MFUKO wa bima ya afya kupitia mradi wake wa KFW umeanza kutoa elimu kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto namna ya kutumia mitandao ya simu kuwasilisha taarifa za afya mama mjamzito na mtoto mchanga.
Hatua hiyo inalengo la kuhakikisha wanapunguza ikiwemo na kuzuia kwa kiasi kikubwa changamoto ya vifo vya wajawazito pamoja na watoto wa changa nchini kote.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mradi wa KFW mkoa wa Tanga Francis Mbwana wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto kutoka katika vituo mbalimbali vya afya mkoani hapa.
Alisema kuwa utaratibu huo wa kutumia teknolojia ya simu katika kusajili na kufuatilia hali za afya za mama wajawazito na watoto zitasaidi kupata taarifa za maendeleo ya afya zao mapema tofauti nasasa.
“Kupitia mradi huu wa KFW muda mwingi fomu za wanachama wapya zilikuwa zinachelewa kutufikia ,huku wakati mwingine mjamzito anakuwa katika hali ya hatari tunashindwa kumfuatilia kwa wakati lakini kupiti njia ya simu tutaweza kufanya malipo na ufuatiliaji kwa haraka”alibainisha Mbwana.
Aliongeza kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha wajawazito wote nchini wanapata fursa ya kujiunga na huduma hiyo hususani maeneo ya vijijini ili kuhakikisha wanapata fursa ya kufaidika na mradi huo.
Nae mmoja wa Wauguzi wa afya Ester Kimweri alisema kuwa toka KFW ianze miaka miatau iliyopita mahudhurio ya wajawazito yamekuwa yakiongezeka kila siku tofauti na hapo awali.
“Mpango wa KFW umesaidia wajawazito wengi kuona umuhimu wa kujifunguali katika vituo vya afya,zahanati na hospitali tofauti na hapo awali mahudhurio yalikuwa ni madogo”alisema Kimweri.
Post a Comment