Header Ads

PPF yatoa elimu ya 'Wote scheme' viwanja vya Mashujaa, Dodoma

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa  akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara wa kilimo cha pamba Riyaz Haider wakati wa akitembelea maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi,  baada ya mfanyabiashara huyo  kupata  mkopo kutoka katika benki kuu ya Tanzania kupitia benki  ya NMB.

................................


Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Mafao yanayotolewa na Mfuko huo.

PPF inatoa Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya, unatoa elimu juu ya mfumo wa ' Wote scheme' kwa sekta isiyo rasmi yaani  wale wanaojiajiri kama vile mama lishe, dereva boda boda, wakulima, wafugaji, wajasiriamali, Wasanii, wote hawa  wanathaminiwa na PPF ndio maana unatoa fursa za huduma  za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na Mafao ya uzeeni.

Kupitia Maonesho haya PPF inasajili wanachama  wapya hapo hapo viwanjani pamoja  na kukabidhi vitambulisho vya  uanachama wa Wote scheme.

Hivyo ni fursa muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja vya Maahujaa kupata elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu ili kufaidika na Wote scheme.


Na kwa wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu  nao

Mkurugenzi mtendaji wa asasi inayochochea uwekezaji sekta binafsi  kwenye kilimo ( PASS ) Nicomedy Bohai akimuelezea mafanikio ya asasi hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  wakati wa maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayofanyika katika viwanja vya mashujaa mkoani Dodoma. 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa cheti kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa udhamini wa Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa  Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio, kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu  Mhe.Jenista Mhagama.

Mzee Seleman Saleh akiwasikiliza Linda Mshana meneja wa mikopo kushoto  na Mary Kapeja mkuu wa kitengo cha masoko na biashara wa UTT Microfince PLC kulia  katika maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi. 

Enock Humba, Afisa matekelezo wa bima ya afya na Grace Michael afisa masoko wa elimu kwa umma wakitoa maelekezo wa watu waliotembelea banda la mfuko wa bima ya afya katika viwanja ya mashujaa mkoani Dodoma. 

Meneja wa PPF wa  Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian akimuelezea kazi za PPF ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko huo  kama vile ' Wote scheme' mmoja wa watu waliotembelea Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga akimfafanulia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matilo fursa zilizomo ndani ya mfumo wa ' Wote scheme' wakati alipotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

Moja ya watu waliojitokeza katika maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kutoka jamii ya wafugaji akiwa katika banda la PPF ambalo wameanzisha mfumo unaotoa fursa kwa watu wote (hata wasioajiriwa) kuweza kuchangia kima cha chini Tsh 20,000 kwa mwezi ambao utamwezesha mchangiaji kupata mafao ya uzeeni na matibabu.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa Mkoa na wawakilishi wa Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi mkoani Dodoma baada ya kufungua rasmi Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

No comments

Powered by Blogger.