Header Ads

Freeman Mbowe, Halima Mdee Wafikishwa Mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge


Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa mbele ya ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge ya kumtaka afike mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matamshi yasiyo na staha aliyoyatoa mapema mwezi Machi 2017 Bungeni Mjini Dodoma yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mhe. Halima Mdee akihojiwa mbele ​​ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kufuatia amri ya Mhe. Spika wa Bunge ya kumtaka afike mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na kutoa matusi Bungeni na kumtukana Spika, matamshi aliyoyatoa mapema mwezi Machi 2017 Bungeni Mjini Dodoma yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.

No comments

Powered by Blogger.