Header Ads

Serikali Kuendelea na Ukarabati wa Nyumba za NHC


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  imesema kuwa Shirika la Nyumba nchini(NHC)  limeweka mkakati wa kuhakikisha nyumba zote zilizo katika hali ya uchakavu zinafanyiwa ukarabati mkubwa na zile ambazo kiwango cha uchakavu ni kikubwa zinavunjwa na kuendeleza upya viwanja hivyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula wakati akijibu hoja mbalimblai za Wabunge leo Mjini Dodoma.

“Shirika la Nyumba la Taifa limeshafanya uhakiki wa nyumba zake zote na kubaini hali halisi ya kila nyumba na kuweka mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba hizo kwa awamu,hata hivyo nyumba ambazo zipo katika hali ya uchakavu idadi yake sio kubwa ukilinganisha na zilizopo katika hali nzuri na bora kimatengenezo”,Aliongeza Mhe.Mabula.

Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 shirika lilitenga takribani shiingi bilioni 11 kwa ajili ya kuzifanyia ukarabati nyumba zake ambapo hadi mwezi Machi, 2017 jumla ya nyumba 2451 zilikuwa zimekwishafanyiwa ukarabati kupitia bajeti hiyo.

Aidha amesema kuwa shirika hilo linatarajia kumaliza ukarabati wa nyumba zote katika mwaka wa fedha 2017/18 na kusisitiza kuwa matengenezo ya nyumba hizi ni kaiz endelevu kwa shirika hivyo bajeti ya matengenezo itaendelea kutengwa kila mwaka ili wapangaji wa nyumba za shirika waendelee kuishi katika nyumba na mazingira bora.

No comments

Powered by Blogger.