Header Ads

Amnesty: China iliwanyonga Watu wengi Zaidi Duniani

 Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limesema idadi ya watu waliopewa adhabu ya kifo imepungua kwa kiasi kikubwa duniani.
Mwaka jana, idadi hiyo ilipungua kwa zaidi ya theluthi moja.
Lakini Amnesty imesema kwamba kiwango hicho hakihusishi Uchina, ambayo inatuhumiwa kuwa na idadi kubwa ya adhabu ya kifo.
Inakadiriwa kwamba, idadi ya waliopata adhabu ya kifo nchini Uchina mwaka jana, ni kubwa zaidi kuliko duniani kote.
Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya muongo mmoja, Marekani haipo katika kundi la nchi tano zinazotumia adhabu ya kifo ambazo ni Uchina, Iran, Saudi Arabia, Iraq na Pakistan.
Nchi ya Belarus na Mamlaka za Palestina zilirejesha adhabu ya kifo mwaka wa 2016. Botswana na Nigeria nazo zilitekeleza hukumu ya kwanza ya kifo mwaka wa 2013.

No comments

Powered by Blogger.