Wanawake Jijini Mwanza Wapatiwa Elimu ya Kujikwamua Kiuchumi
Mtangazaji wa Kipindi cha THE MBONI SHOW kinachoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princes na kurushwa na TBC1, Mboni Masimba, akizungumza kwenye Kongamano la SAUTI YA MWANAMKE lililofanyika jana Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Kongamano hilo lililenga kuwakutanisha wanawake Jijini Mwanza kupata elimu ya kujikwamua kiuchumi katika masuala mbalimbali ikiwemo biashara/Ujasiriamali pamoja na mahusiano katika ndoa.
Mboni alisema Kongamano hilo litakuwa likifanyika kila mwaka kama sehemu ya shukurani kwa watazamaji wa kipindi cha The Mboni Show katika kuwainua wanawake nchini ambapo wanawake mbalimbali waliofanikiwa kimaendeleo wanazungumza na kuwahamasisha wanawake wengine kimaendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, alipongeza kongamano hilo kutokana na elimu inayotolewa katika kumhamasisha mwanamke kimaendeleo ambapo aliwataka wanawake kuendelea kujiunga na vikundi vya kimaendeleo ili kuhakikisha wananufaika na mikopo kutoka halmashauri husika inayotokana na asilimia tano ya mapato yake pamoja na ahadi ya Rais Magufuli ya kutoa milioni 50 kwa kila kijiji/mitaa.

Bi.Chau akiwafunda wanawake Jijini Mwanza.
Mkandarasi Maida Waziri ambaye ni mkandarasi bora mwanamke nchini tangu mwaka 2011 hadi 2015, akiwa pia ni Mkurugenzi wa kamppuni tano, akiwahamasissha wanawake Jijini Mwanza katika suala la kimaendeleo.
Mchekeshaji Katarina Wa Karatu akinogesha Kongamano la Wanawake Jijini Mwanza.
Mwimbaji Zarry Edosha akitumbuiza.
Post a Comment