Makamu wa Rais SAMIA SULUHU aongoza Matembezi ya Hisani Kuchangia Wakunga
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki
mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya
kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground
,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki
mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya
kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground
,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)
akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya
Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya
Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani
,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) na Mkurugenzi Shirika la AMREF Health Africa Dkt. Florence Temu (kulia).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye Matembezi ya
Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye
viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Umati uliohudhuria na kushiriki Matembezi ya Hisani ya Kusomesha Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya
wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.3 ya
kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi,
wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.
Akihutubia mamia
ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground,
Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia
wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya
kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza
vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya
na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote
nchini.
Amesisitiza
kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora
unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa
huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi
na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.
Makamu wa
Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali
katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya
kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika
la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya
Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo
mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye
familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.
Kwa upande
wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema
kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya
wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana
na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya
kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.
Katika
harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo
na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha
wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia
mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.
Post a Comment