Waziri wa Zamani wa
Habari wa Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Zhao
Qizheng akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas
kitabu cha Shanghai Pudong Miracle kinachoonesha
jinsi mji wa Shanghai ulivyotoka kuwa mji wa hali ya chini hadi kufikia mji wa
kisasa na wenye maendeleo, wakati wa kikao kazi cha kubadilishana uzoefu wa masuala
ya Mawasiliano Serikalini baina ya Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini
na Waziri huyo leo Jijini Dar es Salaam.
Akifafanua Mhe. Qizheng amesema kuwa ili Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.
Katika kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.
Pia aliwataka Wasemaji wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazohusu Serikali na wananchi ili kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya haabari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas amesema ni dhamira ya Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea maendeleo.
Post a Comment